Pamoja na kwamba huutumia mkia wake kwa ajili ya kupata balansi, lakini pia huutumia kama mguu mwingine wa tatu.
Je unamfahamu Kangaroo?
- Kangaroo wana ukubwa gani?
- Kangaroo hupatikana wapi?
- Maajabu yao ni yapi?
- Kangaroo wanakula nini?
- Vipi kuhusu kupigana kwao?
- UKUBWA WA KANGAROO
- JE? KANGAROO HUPATIKANA WAPI?
- MAMBO YA KUSHANGAZA KUHUSU KANGAROO
1. HAWEZI KURUDI NYUMA
Kangaroo anashindwa kurudi nyuma kwa sababu mkia wake jinsi ulivyo mkubwa na wenye misuli humfanya hawezi kuruka nyuma.
Watu wa nchi ya Australia ambako Kangaroo ni wengi zaidi, wameichukua hii kama hamasa ya kwamba "Mbele daima, hakuna kurudi nyuma"
2. WANA MAJINA TOFAUTI
Kangaroo dume huitwa boomers, kangaroo wa kike huitwa Flayers, watoto wao huitwa joeys.
Wakati huo huo kundi la kangaroo huitwa mob, troop au court. Kangaroo ni wanyama ambao wanapenda kuwa katika makundi, yaweza kuwa makundi madogo kati ya 3 - 5, au hata makundi makubwa ambao hufika mpaka 100.
![]() |
| Kundi kubwa la Kangaroo |
3. AKIKIMBIZWA HUKIMBILA KWENYE MAJI
Kangaroo si mnyama anayewindwa sana na wanyama, ila mara kadhaa hutokea hata kuwindwa na binadamu hivyo hupenda kukimbilia zaidi kwenye maji.
Lengo la kukimbilia kwenye maji ni kumzamisha adui yake na kuweza kumtoroka. Lakini pia kama ulikuwa hujui kangaroo ni miongoni mwa wanyama ambao hurusha sana mateke. jambo ambalo ni hatari hata kwa binadamu.
4. WENGI WAO HUTUMIA MKONO WA KUSHOTO
Ingawa tumezowea kuona kwa binadamu kuwa baadhi yao hutumia mkono wa kushoto, basi ni vile vile kwa kangaroo wako ambao hutumia mikono yao ya kushoto katika shughuli zao kama vile kulisha na utunzaji wa familia.
5. HAWATOKI JASHO
Kangaroo hawana tezi zinazosababisha jasho. Hivyo hutegemea zaidi kupumzi katika kivuli wakati wa joto.
Wanapohitaji kupata baridi hulamba mikono yao na manyoya yao.
6. UZAZI WA AJABU
Mtoto wa kangaroro anapozaliwa huwa ni mdogo sana kiasi cha kulingana ukubwa na mbegu ya maharage.
"Naaam usishangae ndivyo ilivyo"
Baada ya kuzaliwa akiwa na ukubwa wa nyuki, basi hutambaa katika manyoya ya mama yake mpaka kufika katika mfuko maalum wa mama yake na kukaa hapo kwa ajili ya kukua. Hapo anaweza kukaa hata mwaka mmoja.
Madume hukaa muda mrefu zaidi kuliko majike.
6. ANAWEZA KUSITISHA MIMBA
Kangaroo akishazaa ana uwezo wa kushika mimba kwa mara nyingine. Kisha akaisitisha mimba hiyo mpaka pale ambapo mtoto aliyepo katika kipochi cha mbele kwa mama yake atakapokuwa tayari kutoka na kujitegemea.
Picha ya chini inamuonesha kangaroo jike ambaye yupo na mwanae katika kipochi chake.
7. NI WENGI KULIKO WATU
Hii ni kwa nchi ya Australia ambako hupatikana.
Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika mwaka 2019 ilibainika kuwa na idadi ya watu nchini humo ni milioni 25 wakati idadi ya kangaroo ilikuwa ni zaidi ya milioni 48.
08. MKIA WAKE HUUTUMIA KAMA MGUU
Pamoja na kwamba huutumia mguu wake kwa ajili ya kupata balansi, lakini pia huutumia kama mguu mwingine wa tatu.
Matembezi yao ni ya kipekee, hukita chini mkia wake na kuruka juu. Kwani mkia ni mguu sambamba na miguu yake.
09. HUPIGANA (BOXING)
Kangaroo dume hupigana ili kujua nani mwenye nguvu zaidi na uimara. Hapa kangaroo jike huangalia kuwa ni dume gani imara na kuamini kuwa watoto wao wanaweza kuwa imara pia.
Wanapopigana hushikana kwa mukono yao ya mbele na kupigana kwa miguu. Lakini pia wanao uwezo wa kukita mikia yao na kupigana kwa kutumia miguu yao ambayo ina nguvu sana.
![]() |
| Kangaroo boxing |
10. Kangaroo pia hujipendekeza na kujionesha kwa wanawake wao. Kitendo ambacho hutunisha misuli yao mbele ya mwanamke na atakayekuwa na misuli mikubwa ana uwezekano mkubwa wa kupendwa zaidi.
- KANGAROO WANAKULA NINI?
Kangaroo ni jamii ya wanyama walao majani. Hivyo hula nyasi, mauwa, mwani, wadudu n.k
Soma pia
Makala maalum kuhusiana na radi na mambo ya kuepuka
Nadhani mpaka hapa umepata mawili matatu kuhusu mnyama huyu. Je una kingine cha kuongeza kumhusu? Tuandikie maoni yako hapo chini.




Inaonekana ni mnyama punguani zaydi kuliko wanyama wote mana mwili mkubwa lakini kichwa kama cha panya,lakini pia nyama yake ni nzuri zaydi kulinganisha na wanyama pori wengi mana ina kiwango kidogo cha maduta, likini pia inaonekana ndio wanyama wenye vibamia kuliko wanyama wote mana kama wanazaa viumbe vidogo kama nzi nawaza tu hizo papuchi zao zitakua kama njia ya sindono vile, sasa ikiwa majike ni hivyo vip kuhusu madume yao???.
ReplyDelete😂😁😁😁😁
DeleteKwani tanzania hamna kangaroo jama?
ReplyDeleteNadhani hakuna mkuu
Delete