
Haya ni baadhi ya mambo 10 ambayo hukuyajua juu ya waongoza ndege (pilots) ambayo mara nyingi hufanya ili kujiliwaza na uchovu wa safari ndefu.
1. Kucheza game
Wengi katika marubani hupenda kucheza game zinachochangamsha akili (puzzle) . Tofauti na kuangalia tv ama kusoma vitabu. Vitu ambavyo hupunguza umakini wa ubongo kwa wakati huo.
2. Kusikiliza radio / mziki
Rubani anaweza kujiburudisha kwa kusikiliza music ama kusikiliza radio katika headphone zake ambazo huzitumia kwa mawasiliano na waongozaji ndege walio chini.
Headphone hizo zina uwezo wa kukata music ama radio pale ambapo kuna mawasiliano yamekuja kwa wakati huo.
3. Kujifunza zaidi
Mara chache wanaweza kupata fursa ya kujifunza zaidi. Yaweza kuwa kujifunza lugha ngeni, sambamba na hilo pia wanaweza kuutumia muda huu kwa kujisomea zaidi masomo yao binafsi.
4. Kula
Kama tunavofahamu kuwa marubani hula vyakula vya aina tofauti ili kulinda afya zao ili itakapotokea dharura kwa mmoja wao hasa mchafuko wa tumbo basi mmoja anaweza kulifikisha salama gurudumu hilo.
Hivyo marubani wawapo safarini hula kama watu wengine (abiria)
Lakini yapo mengi ya kushangaza kuhusiana na usafiri wa ndege. Soma makala hii hapa chini kufahamu zaidi.
Soma
Mambo 20 usiyoyafahamu kuhusiana na usafiri wa ndege
5. Hufikiria juu ya hatari zinazoweza kujitokeza
Kama umewahi kupanda ndege bila shaka umeshawahi kuwaza juu ya chochote kibaya ambacho kinaweza kutokea. Ama sivyo?
Basi huko peke yako juu ya hofu hiyo, marubani wako nao huwaza hilo hata pale ambapo hakuna dalili ya hitilafu yoyote. Lazima wafahamu mahala walipo wako karibu na uwanja gani wa ndege ili ikitokea hitilafu wakimbile hapo mara moja ili kuokoa maisha yako.
6. Kubarizi na Kuchungulia dirishani
Ni kawaida kwa abiria awapo kwa muda mrefu katika ndege huchoka na kuamua kugeuza macho yake kutazama anga jinsi ilivyopambwa mawingi yake. Hali kadhalika kwa marubani kufanya hivi zaidi.
7. Umbea kidogo
Kama ilivyo kwa wafanyakazi wowote wenye mafungamano mazuri, lazima kuna muda kazi zinapopungua kuzua umbea wa mawili matatu. Aidha kuhusiana na muajiri wao au vinginevyo,
Marubani nao ni watu kama wewe na kuna muda wanatamani kufanya mambo ya kijamii kama hayo. Sikwambii sasa kwa marubani wa kike.
8. Kupitia ratiba yao ya safari
Kwa sasa i pad imekuwa maarufu kwa marubani. Wachilia mbali matumizi mengine lakini pia huunganishwa na mifumo maalum ya ratiba yake ya ndege. Hivyo wakati akiwa angani kuna baadhi hupitia ratiba yake ya safari na kujua nini kinatakiwa kufanyika katika muda huo au baadaye.
9. Kulala
Ndege ziko tofauti. Lakini baadhi ya ndege kubwa za masafa marefu huwa na vitanda vya siri kwa ajili ya waongoza ndege (pilots)
Vitanda hivi vipo katika vyumba maalum ambavyo havipo mbali sana na chumba cha V I P. Lakini pia mbali na vyumba vya kupumzikia pia zipo bafu, vyoo na kadhalika.
10. Kujipiga picha (Selfie)
Mara nyingi hufanya hivyo pale ambapo wanakuwa huru safarini. Ingawa si ruhusa kwa abiria kuingia kwa rubani (cockpit) ila kwa ruhusa maalum.

Vipi kuhusu picha inayoonekana hapo juu?
Picha hiyo inamuonesha rubani mmoja Raia wa nchi ya Brazi anayejulikana kwa jina la Daniel Contino akiwa ametokeza mwili wake nje akiwa hewani na kujipiga picha. Ukweli wa picha hiyo ni kwamba imefanywa kutengenezwa (photoshop) na haina uhalisia wowote na ni jambo lisilowezekana kabisa.
Umepata mwangaza kidogo? Au una cha kuongezea? Basi usisite kutuachia maoni yako hapo chini
COMMENTS