Hili ni tunda ambalo asili yake ni nchi za kiarabu ambako kuna ukame na jangwa. Mmea wa mtende hufanana sana na mmea wa mnazi au mchikichi. (Tazama picha hapo chini)
Shamba la miti ya mitende |
Tende ni tunda maarufu sana hasa kwa waislamu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani. Hii ni kutokana na ubora na faida zake ambazo hupatikana. Lakini pia ni sunna kuanza chakula wakati wa kufuturu (kufungua) kuanza na tunda hilo.
Kama ndivo, basi unatakiwa ule tunda hili mara kwa mara ili kupata faida ambazo nimeziorodhesha hapa chini.
1. Huongeza nguvu
Tende huongeza nguvu au nishati katika mwili wa binadamu kwa kuliwa kila siku walau tende kuanzia 3. Lakini pia unaweza kunywa juisi yake ni nzuri katika kuongeza nguvu.
2. Huzuia meno kuoza
Mbali na kuzuia meno kuoza na kuyaimarisha lakini pia tende huimarisha mifupa kwa ujumla. Hii ni kutokana kwamba tende zina madini ya manganese, copper na kalshiam kwa wingi
3. Huongeza sukari mwilini
4. Hupunguza kasi ya kupata kiharusi
5. Huongeza nguvu za kiume
Unaweza kuiloweka tende kwenye maziwa ya mbuzi kisha asubuhi unaweza kuchanganya na maziwa hayo na asali na mambo yatakwenda vizuri kabisa.
6. Huimarisha mfumo wa mmengenyo
7. Humsaidia mama mjamzito
COMMENTS