
Huyu ni mdudu maarufu sana majumbani ambaye uwepo wake hunasibishwa sana na uchafu. Hii ni kutokana na mazingira yake ambayo hupatikana kama vile vyooni, jikoni (kuchafu) na hata vyumbani.
Sasa haya ni maajabu yake na mambo ambayo huyafahamu kuhusiana naye:-
1. Kuishi muda mrefu bila kula
Mende ni mdudu ambaye anaweza kukaa kwa muda zaidi ya mwezi mmoja bila kula chochote na bado akiwa hai. Ni wadudu ambao wana uwezo wa kuishi mazingira magumu sana.
Eublaberus posticus ni aina ya mende ambao hawa wanaweza kukaa mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee.
2. Kuishi bila kunywa maji
Wanaweza kuishi kwa muda wa wiki mbili bila kunywa maji
3. Moyo wa mende una chemba 13, wakati moyo wa binadamu una chembe 4 tu.
4. Hawahitaji wanaume ili kuzaliana
Unaambiwa baadhi ya mende wa kike hawahitaji madume ili kufanikisha suala la kuzalisha mayai. Hupandana wao kwa wao na kutaga mayai na maisha huendelea hivyo.
5. Mende ana uwezo wa kukaa kuwa zaidi ya dakika 40 bila kupumua
6. Ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya wiki mbili akiwa hai huku akiwa amekatwa kichwa
7. Hana mapafu
Soma
8. Ana uwezo mara 15 zaidi ya binadamu katika kuzuia madhara ya miale ya nyuklia
9. Ana uwezo wa kuruka kwa maili 3 kwa saa moja.
10. Ana uwezo wa kukaa maeneo yenye sumu na uchafu bila kufa wala kudhurika.
11. Kuna aina takriban 4,600 za mende Duniani. Lakini aina 30 tu ndizo huonekana sana karibu na binadamu wakati huo huo aina 4 ndizo maarufu sana.
Bila shaka umefahamu mambo kadhaa kuhusu mdudu huyu. Una chochote cha kuongezea? Tuandikie maoni yako hapo chini katika sehemu ya COMMENT.
Shukrani kwa makala nzuri kwa kutujuza kuhusu Mdudu mende
ReplyDeleteShukrani kwa makala nzuri kwa kutujuza kuhusu Mdudu mende
ReplyDeleteAsante sana kwa kuwa nasi
Delete