
Wadukuzi ni wataalamu wa mtandao ambao mara kadhaa hujaribu kuingia kwa njia za kitaalamu katika akaunt ya mtu na kufanya uhalifu. Udukuzi huo unaweza kuwa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, instagram, twitter lakini pia barua pepe na hata account za benk.
Burudika na shairi
Pamoja na kwamba kuibiwa account yako yaweza kuwa ni jambo baya, ila kuna aina za password ambazo kama utazitumia ni rahisi sana kwa wadukuzi kukuibia account yako.
Tazama baadhi hapa
1. Namba
Baadhi ya watu hupenda kutumia namba hasa namba ambazo zina mtiririko maalum na ambazo ni rahisi kukaririka ili isiwe rahisi kusahaulika. mfano wa namba hizo ni kama vile 12345, 123123, 987654,
2. Majina
Imekuwa ni kawaida mtu kutumia jina lake kama neno yake la siri. Hii ni rahisi kwa mtu kubuni neno lako na kuweza kukuibia akaunti yako.
3. Maneno maarufu
Baadhi ya watu hutumia maneno maarufu katika jamii kama neno lake la siri. Mfano - i loveyou, welcome, password.
Sambamba na hilo pia baadhi ya watu hutumia maneno ya dini kama vile GOD, ALLAAH, JESUS.
Wengine wakaenda mbali zaidi kwa kutumia matusi makubwa makubwa ambayo nadhani unayafahamu kama maneno yao ya siri katika akaunti zao mbali mbali. Hii ni rahisi kwa mtu kubuni na kupatia.
4. Maneo maarufu
Wengine hutumia maeneo maarufu aidha ya Miji mikubwa, maziwa, majengo maarufu lakini pia hata mitaa yao.
5. Namba ya simu
Nadhani hasa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook watu wengi hasa ambao hujiunga kwa kutumia namba zao za simu badala ya barua pepe hufanya mambo haya.
Anaweza kutumia namba yake ya simu kwa kuweka namba za mwisho au namba za kwanza. Nadhani hii ni njia rahisi zaidi kwa wadukuzi kukuibia akaunti yako.
Soma pia
Mambo 10 yatakayo kushangaza kuhusu kangaroo
Baada ya kusoma dondoo hizi chache unaweza kuchukua hatua kama unaona neno lako la siri linalingana ama kuendana na mada hii.
"Weka neno la siri ambalo unahisi linaweza kuwa la pekee. Unaweza kufanya neno lako la siri kuwa maandishi yasiypfikirika kwa haraka ikifuatiwa na tarakimu"
Udukuzi ni hatari kwani hujui aliyeiba akaunti yako anataka kuifanyia nini, lakini pia anakuwa amekurudisha nyuma kimaendeleo.
Tunaomba maoni yako sehemu ya comment hapo chini kwa ushauri, maoni na mapendekezo.
COMMENTS