Kidogo tulichonacho katika mafundisho ya Mtume tunashea nawewe ndugu yetu Muislamu.
Amesema mtume Wa Mwenyezimungu Rehma na amani zimshukie juu yake.
"Atakapopiga miayo mmoja wenu basi na aweke kiganja chake katika mdomo wake na wala asipige yowe. Kwani hakika shetani humcheka mtu afanyaye hivyo. (anayepiga miayo huku akipiga kelele / mdomo wazi)"
Maelezo ya hadithi hii
Kila kitu kimewekewa adabu yake katika uislamu. Miongoni mwake ni kupihga miayo.
Funika kinywa chako kwa kiganja au hata nguo, na huu ndio ustaarabu hata katika jamii yetu iliyotuzunguka.
Sheitwani ni kiumbe ambaye amelaaniwa na kuwekwa mbali na rehma za Mwenyezimungu, fikiria kiumbe kama huyu akucheke kwa ujinga? je wewe utakuwa mjinga kiasi gani?
Tuyashike mafundosho ya Mtume Muhammad.
COMMENTS