Hadithi ya leo

Amesema mjumbe wa Mwenyezimungu Rehma na amani zimshukie juu yake
"Uislamu ni usafi, basi jisafisheni, hakika haingii peponi ila aliye safi" Hadithi hii imepokelewa na IMAM TWABARANIY
Maezelezo kwa ufupi
Hakuna asiyefahamu umuhimu wa usafi katika maisha. Lakini usafi uliokusudiwa hapa ni aina mbili. Nayo ni usafi wa ndani (moyoni) na usafi wa nje (mwilini)
1. Usafi wa ndani
Huu ndio usafi muhimu zaidi ambao muumini anatakiwa kujipamba nao kwanza. Usafi wa ndani ni kuitakasa nafsi yako kutokana na shirki, hasadi, na mambo yote maovu.
2. Usafi wa nje
Huu ni usafi ambao tunaufahamu, Nako ni kujitwaharisha mda wote kutokana na najisi katika nguo na mwili.
Allaah ndiye mjuzi zaidi
COMMENTS