Amesema Mjumbe wa Mwenyezimungu Rehma na amani zimshukie juu yake
"Watu wawili -Mwenyezimungu hatowatizama (kwa jicho la rehma) simu ya Kiyama.
1. Mwenye kukata udugu. 2. Jirani muovu" (Hadithi hii imepokelewa na Imam Addaylamiy)
Maelezo
Kama kuna hasara kubwa ambayo mwanadamu atakumbana nayo siku ya kiyama ni kutotazamwa na Allaah.
Mwenye kukata udugu ni miongoni mwa watu hao. Kukata udugu ni jambo baya na Mtume ametukataza kwa makatazo makali sana.
Na Mtume ametuusia kuwatendea wema majirani zetu hata wasiokuwa waislamu.
Allaah ndiye mjuzi zaidi.
COMMENTS