Maoni yako ni ya thamani kwetu kuliko unavyodhani. Tuandikie hapo chini baada ya kumaliza kusoma makala hii itakayokunufaisha

______________
Kwa wanaume walio wengi suala la kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni ngumu kueleza namna hali hii ilivyo kwao, lakini pia sambamba kwa wanawake baadhi yao ni vigumu kuelezea hasa wawapo na wapenzi wao.
Hii ni kutokana na hofu ya kuonekana kuwa hawawapendi wapenzi wao au kuonekana wana mapungufu.
Hapa nitakueleza dalili za mtu ambaye anakosa hamu ya kufanya mapenzi kwa undani kabisa.
Hivyo maana halisi inaweza kupatikana baada ya kusoma dalili zake hapa chini.
Namna ya kutambua kuwa una tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi
Hali ya kukosa hamu ya kufanya mapenzi si tatizo linalojitokeza kwa ghafla kama inavofikirika kwa wengi ambapo unaamka asubuhi moja kwa moja na kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Hii ni suala ambalo linajikuza taratibu kwa kipindi kirefu.
Ni vigumu kulipima tatizo hili kwa kuwa kiwango cha uwingi wa matukio ya kufanya mapenzi baina ya wapenzi si kipimo cha kuwa au kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi kwani kuna mambo mengi yanaweza kuingilia matukio hayo ya kufanya mapenzi mfano kuumwa, mzunguuko wa hedhi kwa mwanamke, ujauzito na kadhalika.
Je? Sasa nitajuaje kama unakosa hamu ya kufanya mapenzi?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo yakiwa kwa mmoja wenu huenda kuna dailili ya kukosa hamu ya mapenzi;-
1. HISIA na KUGUSANA
Je? Kugusana kwenu ni kwa kawaida au ni mpaka pale mnapoingia chumbani?
Kama wapenzi si suala geni kushikana mikono, kugusana, kukumbatiana hata wakiwa barabarani au sehemu nyingine yoyote bila kujali watu watawachukuliaje.
Lakini ikiwa hali hii inafanyika tu mkiwa ndani wakati wa tendo tu basi hapo kuna dalili hiyo (mmoja kutokuwa na hamu).

2. TENDO la NDOA
Ikiwa kufanya kwenu mapenzi hakuwafanyi kuungana na kuwa kama kitu kimoja na kuwafanya kuoneshana ufundi ili kuridhishana kama ilivyokuwa hapo zamani.
Hii ni ile hali ya kuwa unataka tu kujiridhisha wewe mwenyewe bila kujali hisisa za mwenzi wako.
Ukifika katika hali hii jua wazi kuwa ni dalili ya kukosa hamu ya tendo la ndoa.
3. MUOMBAJI / MLAZIMISHWAJI
Hii hutokea pale ambapo mmoja wenu tu ndiye anayeomba kufanya mapenzi na mwingine akiwa kama analazimishwa.
Soma pia Mazoezi 6 yanayo ongeza nguvu za kiume
4. KUACHA KUTARAJIA KUFANYA MAPENZI
Ziko siku ambazo ni spesho, inaweza kuwa ni harusi ya ndugu au jamaa, sikukuu na kadhalika.
Siku hizi wapenzi huwa wanajiandaa na kupendeza na kuamsha hamu kubwa ya kufanya mapenzi tofauti na siku za kawaida. Kubadilisha mazingira na mambo mengine mengi ambayo hujikuta yanachochea hamu.
Lakini kwa wapenzi ambo wamekosa hamu ya mapenzi hili jambo linabaki kuwa ni stori.
5. MAPENZI KUWA SEHEMU YA WAJIBU
Hapa ni pale ambapo wapenzi hufanya mapenzi kwa sababu ya kutimiza wajibu tu aidha kwasababu wameoana au kwasababu ni kawaida.
Hapa ni pale ambapo unafanya mapenzi ya ulienaye kwasababu tu asije akakuacha au asije akawa na maswali mengi juu yako.
Je nisababu gani hupelekea mtu kutokua na hamu ya kufanya mapenzi?
Ziko sababu nyingi ambazo humfanya mtu hukosa hamu ya kufanya mapenzi na mpenzi wake. Na sababu hizi hutofautiana baina ya mwanamke na mwaname na kuna zile ambazo huoana.
Sababu hizi zipo kwenye makundi matatu;-
- Sababu za kisaikolojia
- Sababu za kiafya
- Sababu za kitabia
- Tiba sahihi
Wacha tuzichambue kundi moja moja
1. SABABU ZA KISAIKOLOJIA
KWA MWANAMKE
Wasi wasi (Anxiety)
Hii ni ile hali ya mtu kuwa na woga na mawazo mengi kutokana na mambo yanayofahamika au yasiyofahamika kwa urahisi. Lakini yanakuwa ni matatizo yanayomsibu au kumkera kila wakati bila kikomo.
- Kwa mwanamke mawazo haya yanaweza kutokana na afya ya watoto, wazazi au ndugu wa karibu, tabia mbaya za mume wake kama vile ulevi, kupigwa au umalaya.
- Lakini pia kuogopa ndugu wa mume walio wakorofi, usafi mdogo wa mume kama vile kutokuoga, kutonyoa nywela na ndevu nguo chafu, kutopiga mswaki na mengineyo.
- Kutojali hisia za mwanamke chumbani alizonazo. Yaani kutomuandaa mwanamke ipasavyo na mwanamke kujiona ni kama chombo tu cha starehe.
- Lakini pia suala la kutomjali mwanamke nje ya nyumba na kumdhalilisha mbele ya watu kwa namna yoyote ile. Kama vile kumtukana, kumpiga. Haya ni mambo yanayompa mwanamke wasi wasi na kiuutotamani kufanya mapenzi nawe kwa hisia.
- Hofu nyingine ni juu ya maumbile ya mwili wake kwa kuhofia kuwa huenda usimvutie mwenza wake. Vitu kama maumbile ya matiti yake aidha kuwa makubwa sana au madogo sana au kuwa yameanguka sana. Hali kadhalika maumbile ya sehemu zake za siri na viungo vingine.
- Mwanamke kutompenda mwanaume aliyenaye kwa sababu ya kuingia kwenye mahusiano kwa kulazimishwa.
- Kubadilika kwa kipato kwa mwanaume. Huenda hapo awali mwanaume alikuwa na hali nzuri kiuchumi lakini baadaye akaja akayumba na mwanamke hakuwa amezoea hali hii. Hii pia huwaathiri baadhi ya wanawake ki saikolojia.
- Lakini pia kupanda kwa hadhi ya mwanamke hususani kazini. Baada ya kupanda hadhi / cheo na kukutana na watu wenye hadhi ya juu zaidi ya mume aliyenaye pia inaweza kuwa ni sababu ya kumpuuza na kutokuwa na hamu naye ya mapenzi.
KWA MWANAUME
Matatizo ya kazi
Mawazo ya kukosa kazi, kuachishwa kazi, migogoro ya kazini hali kadhalika na ugumu wa majukumu ya kazi.
Mambo kama haya huwa yanamfanya mwanaume afikirie sana na kutumia nishati nyingi katika kupambana na hali hizo. Mambo hayo huufaya mwili kukosa nafasi ya kutulia na kuwaza tendo la ndoa na mwanamke aliyenaye
Mwanamke kuwa msemaji sana
Kama hujawahi kukutana na hii basi ushawahi kusimuliwa na rafiki yako.
Mwanamke msemaji kupita kiasi, mkosoaji wa kila jambo, asiye na shukrani na asiye na kauli nzuri ni kikwazo kikubwa sana kwa mwanaume kiasi cha kumkata hamu yake ya mapenzi.
Mwanaume hupenda mwanamke mwenye kauli laini hata pale anapokuwa analalamika au kumkosoa ni vema kutumia lugha ya upole.
Mwanamke asiyeridhika
Hasa kutoridhika na kipato cha mwanaume, manung'uniko yasiokwisha juu ya hali yao ya kimaisha.
Mwanamke mwingine humlinganisha mwanaume wake aliyenaye na mwanaume mwingine mwenye kipato zaidi yake kwa kudhani kuwa atamfanya ajitume zaidi kumbe ndio anazidi kumnyong'onyeza.
Mwanamke kutotulia katika mahusiano
Mwanamke ambaye anaonesha tabia zisizo eleweka kwa uwazi. Jambo hili humpatia mwanaume mawazo yasiyokwisha ambayo humfanya asiwe na hamu ya mapenzi na mwanamke huyo.
Mfano mzuri ni mwanamke ambaye anapenda sana kuongea na simu na wanaume wengine kila mara huku mume wake akisikia. Wakati huo mazungumzo hayo yakiwa ni ya kawaida kabisa na sio ya kikazi wala ki biashara.
Mwanamke kuwa na tabia ya kuwa na marafiki wengi wa kiume na hata kutoka nao kwenda sehemu zisizo eleweka.
Mwanaume kutovutiwa na mwanamke
Hii ni kutokana na kutovutiwa na mwili wa mwanamke kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kulazimishwa kuingia katika mahusiano hayo.
Kulazimishwa huku kunaweza kuwa ni sawa na ile tuliyoisema hapoi juu katika sababu za mwanamke. Lakini pia mazingira yanaweza kumsababisha mtu kuingia katika mahusiano ambayo hakuyaridhia. Mazingira hayo yaweza kuwa ni kipato au umasikini pia.
2. SABABU ZA KIAFYA
Sababu hizi za kiafya pia zimetofautiana baina ya mwanamke na mwanaume. Hapa tumechanganya kwa wote.
1. Vidonge vya uzazi wa mpango
Hivi ni vile vidonge vya kawaida vinavyotumika katika kuzuia kupatikana kwa ujauzito kwa mwanamke.
Baada ya kumeza vidonge hivi husagwa katika ini na kuzidisha kiwango cha protini katika damu ambayo inazuia vichocheo vya testosterone ambayo husaidia kuamsha hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake na wanaume pia.

2. Madawa makali
Dawa nyingine zinazoweza kupunguza uwezo wa mwanamke kuwa na hamu ya kufanya mapenzi ni zile ambazo ni kali au zinazotumika kwa muda mrefu na kuufanya mwili kuwa na uzalishaji mdogo wa vichocheo vinavyoongeza hamu ya mapenzi.
Dawa hizi ni kama zile za shinikizo la damu, dawa za kupunguza mfadhaiko na dawa nyingine zinazotumiwa kwa muda mrefu kama vile dawa za kansa.
3. Uchovu uliopitiliza
Endapo unafanya shughuli ambazo zinakufanya uchoke sana, ngono haiwezi kuwa kitu unachotamani kukifanya.
Hii ni kwakuwa mwili unakuwa umeelemewa kupita kiasi na kazi kiasi kwamba unakosa nguvu za kuzirudisha hisia za mapenzi.
4. Kisukari
Ugonjwa wa kisukari unasababisha aina fulani ya matatizo yanayohusiana na maswaka ya kimapenzi kwa asilimia 50 ya wanaume na asilimia 25 ya wanawake wanaougua ugonjwa huu.
5. Endometriosis
Hii ni hali ya kiafya inayowapata wanawake pale ngozi ya ndani ya tumbo la uzazi inapokuwa imetoka na kujikuza nje ya tumbo la uzazi.
Ngozi hii ama utando huu unaweza kukua na kuweza kufunika seheu ya nje ya tumbo la uzazi, sehemu ya ndani ya nyonga, mirija ya mayai ya uzazi na kibofu cha mkojo.
Mwanamke kila anapopata hedhi utando huu hukuwa zaidi na kusababisha uvimbe, kuvuja damu, nyama kuganda na kufayika kwa kovu.
Wanawake wenye tatizo hili wanaweza kuugua kwa miaka mingi endapi wasipopimwa mapema na kugundulika.
Dalili za tatizo hili ni maumivu makali wakati wa hedhi na inasemekana kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye kupatwa na maumivu makali ya hedhi wana tatizo hili.
Hali hii humuathiri mwanamke kufanya kazi zake za kawaida na hata uwezo wake wa kufanya mapenzi.
6. Umri
Wanawake wanapoelekea kwenye umri ambao hedhi inakoma, mayai yao yanaacha kuzalishwa na pia hormone za estrogen na testosterone zinaacha kuzalishwa na uke unaanza kusinyaa na uwezo wao wa kupata hamu ya kufanya mapenzi nao unapungua kama sio kuisha kabisa ingawa inasemekana kwa baadhi yao uwezo wao ndio unaongezeka.
Kwa upande wa wanaume umri huwaathiri kwakuwa uzalishaji wa hormone za mapenzi unashuka na kuwa wa taratibu na kufanya hamu ya kufanya mapenzi iwe inakuja kila baada ya muda mrefu badala ya kila baada ya muda mfupi.
Hua sipendi nikuchoshe katika makala zangu, hivyo kwa leo tutaishia hapa.
Lakini tumebakisha sababu za kitabia ambazo humfanya mtu kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Baada ya kusoma sababu hizo, na sasa tunamalizia 'sababu za tabia' ambazo ndio za mwisho.3. SABABU ZA KITABIA
1. Ulevi kupindukia
Matumizi makubwa ya ulevi au alcohol ni jambo ambalo linaweza kusababisha upungufu wa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke au mwanaume.
Ingawa kuna wanawake wanadai kuwa wanapolewa ndipo hupata hamu zaidi ya kufanya mapenzi pia lakini uhalisia uko hivyo.
Kwa vile hormone ya testosterone inawezesha hamu ya mapenzi na kusisimka kwa viungo vya uzazi, pombe ina kawaida ya kuwa na madhara ya kupunguza utendaji wa viungo vya uzazi vya wanaume.
Sambamba na hilo pia utafiti unaonesha uwa pombe inapunguza hormone ya testosterone ambayo huchochea hamu ya mapenzi.
Kingine ni kuwa pombe inapunguza hisia za raha anayoweza kuipata mtu wakati wa kufanya mapenzi. Inapunguza ukubwa wa hisia anazozipata mtu hata wakati anapofika kileleni na kuingilia uwezo wa mtu kufika kileleni.
Kwa upande wa wanawake walio wengi, pombe inaongea kusisimka na hamu ya kufanya mapenzi ila ingawa inaongeza kusisimka na hamu inazuia kuonekana kwa dalili za kusisimka huko.
Dalili hizo ni kama vile kulainika kwa uke na kutoa maji maji ya kutosha.
Pamoja na hayo pombe inawadhuru wanawake kwa namna tofauti pia.
2. Sigara
Uvutaji wa sigara pia husababisha upungufu wa hamu ya kufanya mapenzi hasa kwa wanaume.
3. Punyeto
Huenda ikawa punyeto ikawa haina madhara makubwa katika kuwa na hamu, ila ina mchango mkubwa katika kumfanya mtu kutotamani kufanya mapenzi kutokana na kutojiamini.
Soma Madhara ya kupiga punyeto kwa muda mrefu
SULUHISHO LA TATIZO HILI
1. VYAKULA

2. TIBA YA MAZOEZI
COMMENTS