Zana hizi zinakutosha sana kumiliki blog tena ya kisasa kabisa....

Ipo mitandao mingi ambayo inatoa huduma za blogging, miongoni mwao ni blogger.com, wordpress.com, joomla na kadhalika.
Kila mtandao una utaratibu wake wa kujiunga, lakini leo nitazungumzia kuhusu mtandao huu wa blogger ambao ndio nautumia.
Hizi ni hatua za kufuata.
1. Fungua email akaunt ya gmail
Kama tayari una akaunt ya gmail basi ni rahisi sana kujiunga na Blogger. Gmail na Blogger yote ni mitandao inayomilikiwa na Google.
Wakati wa kujiunga itakuletea mfano wa maneno ambayo nimekuwekea baadhi ya picha hapo chini. Lugha itategemea na jinsi ulivoweka katika kivinjari chako.
![]() |
| Hatua ya kwanza |
![]() |
| Hatua ya pili |
Fuata utaratibu kama ambavyo utaelekezwa. Baada ya kukamilisha utaratibu wa kujiunga na email ya google, sasa utakuja hatua namba mbili.
2. Jiunge na Blogger
Baada ya hapo utajiunga na Blogger kwa kufuata hatua ambazo watakuelekeza. Kisha utaweka jina lako ambalo utahitaji litumike katika blog yako.
Niwe na nini ili niweze kuendesha blog yangu?
Ni kuwa tu na kifaa ambacho utaweza kuingia katika blog yako na kuweka machapisho. Kwa jibu rahisi ni kwamba unaweza kublog kwa kutumia simu yako tu.
Lakini kama unataka blog yako iwe bora zaidi ni lazima uwe na vifaa hivi;-
1. Computer
Hili ndilo hitaji kubwa kwa ajili ya kuendesha blog. Ni vema ukatumia laptop kwa sababu mbali mbali ikiwemo;-
- Ni rahisi kubebeka
- Inatunza chaji
Lakini kama utakuwa una blog ukiwa ofisini kwako tu na unatumia UPS kwa ajili ya kutunza chaji pindi umeme utakapo katika basi unaweza kutumia desktop.
Ingawa unaweza kublog kwa kutumia simu, lakini hushauriwi kwasababu kuna baadhi ya mambo utashindwa kufanya au utafanya kwa taabu.
Vifaa vingine vitategemea na aina ya blog yako kama utajihusisha na nini? Kama ni blog ya picha unahitajika kuwa na camera au simu yenye uwezo wa kupiga picha nzuri.
2. Camera
Hata kama blog yako haihusiani sana na picha lakini kuna baadhi ya machaposho utahitajika kuweka picha ili kupendezesha. Na ni vizuri kuweka picha ambayo inaleta uhalisia na yenye ubora mzuri.
Haya ni mambo ya kufanya ili uandike makala bora
Soma Njia za uandishi wa makala bora
3. Notebook na Kalamu
Kuna muda unaweza kupata wazo la kuandika na ukawa mbali na laptop yako. Pia ni vema kabla hujaandika katika ukurasa wako wa blogger kuandika wazo lako katika notebook yako.
4. Muda
Unaweza kuwa na vyote hivyo hapo juu na usifanikiwe kwa kukosa muda wa ku blog.
Muda ni rasilimali muhimu sana katika kuhakikisha unaandaa kitu ambacho wasomaji watapenda.
Bila kuwa na muda au muda wa kutosha unaweza kuambukia patupu.
Hitimisho
Hizi ni zana muhimu za kuanzia kama unataka kufanya kazi ya blogging. Lakini huenda wewe unapenda sana kuanzisha blog au youtube channel na unashindwa kuwa na MADA maalum ambayo utakuwa unazungumzia hasa.
Hizi hapa ni Idea bora kwa wanaotamani kuanzisha blog au channel ya youtube.
Soma


COMMENTS