Mteke mtazamaji akufuatilie kila siku kwa mbinu hizi 10

Hivyo basi, nami ni miongoni mwa ambao watazifanyia kazi mbinu hizi ambazo nitakueleza hapa ili kukuza channel yangu ya youtube (Bunduki TV)
Kwakuwa sipendi kuwa mchoyo nimeona nikushirikishe nawe msomaji wangu, basi nawe mshirikishe mwingine na mwingine amshirikishe mwingine ili sote tufike lengo.
Hizi ni 'Njia sahihi za kukuza youtube channel yako ndani ya muda mchache".
1. Chapisha mara nyingi kwa wiki
Takwimu zinaonyesha kuwa, miongoni mwa channel ambazo hufuatiliwa sana ni zile ambazo zinaweka machapisho mengi kwa muda mfupi.
Chapisha walau mara tatu ndani ya wiki moja. Hii inachangamsha channel yako na kumfanya hai mtazamaji wako anaye kufuatilia.
2. Mwanzo unaovutia
Anza na kipande ambacho unahisi kinavutia. Ni vema sana mwanzoni mwa video yako kuweka kipande ambacho kinavutia. Hii humvuta na kumshawishi mtazamani kuitazama video yako yote ili asikose uhondo huo.
Tumia chambo kumvuta mteja wako.Lakini hakikisha kipande unachokiweka kinaendana na mada husika.
Usiweke kionjo cha video nyingine, hii utamfanya mtumiaji kutorudi tena kwasababu ya uongo wako.
Yafahamu Makosa 10 wanayoyafanya youtubers
3. Mwanzo mfupi
Karibu kila channel huanza na ufunguzi wa kuitambulisha, hili ni jambo jema sana.
Kitu muhimu cha kuzingatia ni kujitahidi mwanzo huo usiwe mrefu kuzidi sekunde 10. Hii haita mchanganya na kumchosha mtazamaji wako.
4. Ongeza screen (mwishoni)
Hii ni njia nzuri ya kutangaza video zako nyingine ambazo umeshazipandisha youtube.
Mtu atakapomaliza stori anayoitazama ataletewa video nyingine ambazo kama zitamvutia atazitazama pia.
Mbali na end screen unaweza kuongeza card kati kati ya video ili baadaye mtu aweze kuvutiwa nazo.
Tazama kielelezo hiki👇

5. Epuka uongo na ujanja ujanja
Unatakiwa kuweka thumbnail ambayo itamvutia mtazamaji. Lakini epuka kuweka thumbnail ambayo itamdanganya mtazamaji.
Mtu unapomvutia kwa habari za uongo hatokupenda na hatotamani kurudi tena katika channel yako.
Hali kadhalika katika mtiririko wa habari zako epuka ujanja ujanja usio na maana.
6. Weka video ndefu
Masaa mengi ya kutazamwa katika channel yako ni bora zaidi kwani ndivo vigezo muhimu kwao (youtube).
Uwekaji wa video ndefu ni njia nzuri ya kuongeza masaa ya kutazamwa kuliko video fupi. Video yenye dakika 20 haiwezi kulingana na video ambayo ina dakika 2 au 3.
7. Nenda LIVE (Streaming)
Kwenda moja kwa moja (LIVE) youtube ni njia nyepesi ya kufikisha maudhui yako bila kutumia nguvu nyingi katika kuhariri na kupakia (Uploading).
Lakini pia kwenda live ni njia rahisi ya kuwasiliana na wateja wako moja kwa moja. Lakini pia mbali na hayo ni njia nzuri sana ya kuongeza masaa ya kutazamwa.
8. Weka mtiririko
Huwa inapendeza mtu anapofuatilia jambo moja mpaka mwisho kabla ya kuingia kwenye jambo lingine.
Pandisha video zako katika mtindo wa mtiririko maalum ili kutowapa shida watazamaji wako.
Kuwa na playlist pia ni moja ya njia nzuri za kuhifadhi video zako kitaalamu zaidi.
9. Shirikiana na youtubers wengine
Nukta hii tuliiona hata katika njia zinazoweza kuimarisha blog yako
Hapa unatakiwa kushirikiana vema na watengeneza maudhui wenzako. Huenda baadhi ya watu hawaijui channel yako lakini kupitia kuonekana kwa mwenzako baadhi ya watu watakufuatilia.
10. Weka logo
Isiwe logo yenye kukera kama tulivo zungumza katika mambo ambayo watu youtube hukosea sana.
Mara kadhaa watu hudownload video na kuzipost katika mitandao mingine ya kijamii kama vile instagram, facebook na hata tiktok.
Kuweka logo kutasaidia wewe kutambulika na mtu ambaye ameiona video ile sehemu nyingine.
Ziada yangu ni kukuomba wewe kuweka maoni yako sehemu ya chini ya comment.
Je makala hii imekusaidia?
Asante kwa kuwa nasi.
Shukran
ReplyDelete