Mara nyingi watu wanashea nasi maisha yao binafsi, vivutio vya watalii, kazi zao na mengine mengine katika mfumo wa video. SI UMEWAHI KUONA HII?

Wakati huo huo VLOG ni njia ya kuweka maudhui (binafsi) mtandaoni kwa njia ya video.
Hivyo tofauti kati ya maneno hayo mawili ni namna ya uwasilishaji (maandishi na video)
Kwa upande wa vlog watu huutumia sana mtandao wa youtube kwa kuweka video.
Kwakuwa watu wametofautiana, wapo ambao wanapenda kusoma na ambao ni wavivu wa kusoma wanapenda kutazama zaidi. Hivyo ukiwa kama mtu ambaye unapenda kutoa maudhui mtandaoni ni vema kuangalia aina ya wateja wako.
VIFAA VYA KUWA NAVYO
Tunaihusisha sana Vlog na blog kwa sababu ni vitu ambavyo vinaendana.
Ili kufanya vlog kitu kikubwa cha kuwa nacho ni kifaa ambacho utaweza kuchukua video tu. Lakini kama ungependa na sauti isikike basi unaweza kuwa na kifaa ambacho kinaweza kuchukua video na audio.
Hapa utagundua kuwa simu yako (smartphone) inatosha sana kufanya vlogging.
___________
Lakini hizi ni zana ambazo unatakiwa kuwa nazo kama unataka kufanya vlogging kitaalam zaidi.
1. CameraKama ukihitaji kupata video ambayo watu watapenda zaidi ni wajibu upate camera ambayo utapata video nzuri zaid (HD)
Mimi natumia camera aina ya canon EOS M50 ambayo ina uwezo wa kupiga picha bora kabisa (4K) na ni camera ndogo ambayo unaweza kuiweka hata katika mfuko wa shati.
2. Microphone
Camera nyingi huwa zinakuwa na mic yake (built in microphone) lakini kama unataka sauti ambayo itakuwa bora zaidi tumia chanzo ambacho ni bora zaidi cha sauti (audio).
Kama kamera ulionayo ina port ya mic basi tumia mic ya nje ambayo itakuwa bora na kukupa kile ambacho watu watapenda.
Kama camera yako haina mic pot basi unaweza kutumia chanzo kingine cha sauti ambacho kitakuwa vema. Unaweza kutumia mp3 recorder, simu n.k.
3. Laptop / computers
Ingawa unaweza kutuma video yako moja kwa moja bila ya kuifanyia edinting yoyote, lakini kilichobora zaidi ni kuihariri video yako na kuongeza baadhi ya vitu kama vile rangi, logo, maandishi n.k.
Hapa ndipo umuhimu wa laptop / computers unapokuja. Sambamba na hilo pia lazima uwe na program nzuri kwa ajili ya video editing. Unaweza kutumia Sony vegas, Adobe premier na nyinginezo.
4. Stand ya camera
Stand ya camera itakusaidia kutuliza camera pale ambapo unataka kuchukua video ambayo inatakiwa kuwa na utulivu.
Kwa video ya muda mrefu unapotumia kushika camera kwa muda mrefu ni lazima utachoka na pia picha itakuwa inacheza cheza.
Zipo stand za aina nyingi, za miguu mirefu na miguu mifupi. Hapa itategemea na umuhimu wako.

5. Taa
Yote haya ni katika kutafuta kitu ambacho kitakuwa ni bora kabisa. Kuna video ambazo huenda ukachukua usiku au sehemu ambazo mwanga ni mchache lazima uwe na taa ya kurekodia.
6. Gimbo
Gimbo hutumika wakati umeamua kupiga picha za video kwa mkono. Gimbo ni kifaa ambacho kinakusaidia kuufanya muondoko wa video yako (motion) kuwa laini (smooth) na wenye kuvutia.
Hata kama ikitokea umepeleka mkono kwa haraka, video ingetakiwa kuharibika lakini kwa kutumia gimbo video itaendelea kuwa laini ya yenye kuvutia sana.
7. Camera man
Mpiga picha ama mtu wa kushika camera wakati unapo record ni muhimu hasa pale ambapo utakapokuwa mkubwa.
Unaweza kushika kamera mwenyewe na kutoa maudhui, lakini ili kuwa huru zaidi ni lazima uwe na mtu nyuma ya camera.
JE? NIFANYE VLOG AU BLOG?
Huenda apo ulipo unajiuliza kuwa ni kipi bora kati ya Blog au Vlog?
Swali hili halina jibu la moja kwa moja ila kwa sasa kuna idadi kuwa yatu ambao hufuatilia video zaidi kuliko kusoma.
Hivyo, kama maudhui yako ungependa yatazamwe badala ya kusomwa, ama wewe ni mvivu wa kuandika ni vema kufanya vilogging (video blogging).
Lakini kikubwa kuliko vyote ni NICHE / IDEA ambazo unataka kutembea nayo.
Niche maana yake ni fungu la maudhui ambayo unataka kuzungumzia katika vilogging yako.
Soma: Idea bora 26 kama unataka kuanzisha Vlog
Umetamani kufanya vglogging?
Tuandikie maoni yako hapo chini sehemu ya comment

COMMENTS