Elimu ndio msingi wa kila kitu, elimika kisha waelimishe na wengine waliyo tayari

Leo katika kipengele cha Blog tips / mbinu za blog nitakudokeza kuhusiana na kitu ambacho kinaitwa DOMAIN ama kwa kiswahili unaweza kuita Kikoa.
Katika safari hii ya dakika mbili tu, nitakupitisha katika njia hii;-
1. Domain ni nini?
2. Kwanini uwe na domain ya kulipia?
3. Nawezaje kupata domain?
4. Faida ya domain
5. Hitimisho
"Kumbuka tu maoni yako ni ya thamani sana kwangu, hivyo kwa chochote ambacho umekiona katika makala zangu naomba uniwekee maoni yako hapo chini katika sehemu ya comments".
1. DOMAIN NI NINI?
Domain ni anwani / jina ambalo hutumika katika mtandao. Ni sawa na namba ya simu katika mawasiliano ya kawaida.
Hapo awali ilikuwa ili kuingia katika website ni lazima uandike IP Adress. Baada ya kuona tabu iliyopo ndipo wataalamu wakagundua domain name (Jina la kikoa) mfano mrbunduki.com na kadhalika.
Pia kuna aina nyingi za domain kulingana na matumizi na eneo la website husika. Zipo ambazo zinaishia na .co.tc / .web / .tech / .com na kadhalika.
NUKUU
Domain ni moja tu duniani kote, haiwezekani kujirudia kwa mtu mwingine.
2. NAWEZAJE KUPATA DOMAIN?
Domain zipo za zina mbili. Zipo ambazo zinapatikana bure na zipo ambazo ni za kulipia.
Kwa domain za bure huwa zinakuwa na jina la mtandao husika ambao umeisajili blog ama website yako. Baadhi ya mitandao hiyo ni kama vile blogger, wordpress, joomla na kadhalika.
Hivyo kama hujalipia domain, jina lako litakuwa limeambatana na jina la mtandao husika. Mfano mrbunduki.blogspot.com
Aina ya pili ya domain ni ya kulipia. Hapa ndipo unaweza kupata jina lako ambalo unalitaka na kuondoa kile kikoa cha mtandao. Na blog yako itakuwa kama hivi mrbunduki.com
3. KWANINI NILIPE DOMAIN?
Hii ni kuifanya blog / website yako kuwa ya kitaalamu na ya kupendeza zaidi. Ili uonekane kweli unajua unachokifanya kwanza kabisa mtu atataka kujua jina la blgo yako.
Hata mtu anaopotaka kutangaza katika blog yako ni lazima aangalie vigezo vingi sana kabla ya kuamua kufanya hivyo. Domain ya kulipia ni miongoni mwa vigezo vikubwa sana.
Soma makala hii;-
4. NAWEZAJE KUPATA DOMAIN YA KULIPIA?
Ipo mitandao mingi tu ambayo unaweza kupata kulipia domain. Miongoni mwa hiyo ni pamoja na google domains, go daddy, domain.com na kadhalika.
Kiasi cha chini kabisa unaweza kulipia kwa mwaka mmoja ambayo hugharimu kuanzia Dola 8 - 20 na kuendelea. kwa pesa Tanzania ni shilingi elfu 18 hadi 45 kwa mwaka. Nadhani ni rahisi ee?
Kila mtandao una sheria na taratibu zake za kulipia, lakini kwa asilimia kubwa utalipa kwa Mastercard au Visa.
5. NI IPI FAIDA YA DOMAIN
Faida zipo nyingi, lakini hizi ni miongoni mwa chache zenye nguvu ambazo nimekuwekea hapa chini.
i. Kuifanya blog yako kuwa ya kijanja
Kama unatumia Domain / kikoa cha mtandao bado wewe sio mjanja. Na kwa wanaojua mambo haya atakuona bado haupo serious na kazi yako.
ii. Blog yako itavutia
Mbali na kuvutia kwa jina lako ambalo umelichagua kuwa la kipekee, lakini pia mtu akiona una domain ni rahisi kumvutia na kuendelea kusoma makala zako.
Bila kusahau kuwavutia wawekezaji ambao huenda watahitaji kufanya kazi nawewe. Hii ni faida kubwa ambayo kila mwana blog anataka kuipata.
iii. Kuwa wa kipekee
Hii inakutofautisha wewe na bloggers wengine, ni kama vile jina lako binafsi. Ni vizuri zaidi kuchagua jina ambalo ni rahisi mtu kujua blog yako inajihusisha na nini. Kama ni mtu wa michezo, burudani, afya na mengineyo.
Au kuipa jina ambalo huenda hakuna mtu mwenye jina kama hilo. Ubunifu ni kitu kizuri katika kazi yoyote.
HITIMISHO
Blogging ni kazi kama kazi nyingine, blogging ni bure lakini ili uwe blogger bora duniani ni lazima uwekeze gharama stahiki ili kuendana na kasi ya ulimwengu.
Miongoni mwa gharama hizo ni pamoja na kununua domain yako ambayo utaimiliki mwenyewe.
Usikate tamaa mafanikio yatakuja muda si mrefu. Tuendelee kuelimishana na kupeana ujuzi ili tufike tunapokusudia.
UWE NA SIKU NJEMA
COMMENTS