Kitu bora ni kile ambacho kinakuingizia chochote cha faida kwako
_____________
Bila shaka utaungana nami kuwa ni ndoto ya kila mwana blog kupata pesa kupitia blog yake. Ingawa kwa sasa atakwambia kuwa anafanya kama hobby au mapenzi tu.
Lakini ukweli ni kwamba kila mtu ana matarajio juu ya kuingiza pesa kupitia blog yake.
Kama ndivyo, hapa nimekuandalia njia 5 tu ambazo unaweza kupata pesa kupitia blog yako.
1. Tafuta matangazo binafsi
Wengi wao wanafikiria kufanya matangazo na makampuni makubwa hapa nchini na nje ya nchi kama vile mitandano ya simu, makampuni ya vinywaji, bank na kadhalika.
Hii ni hatua ambayo kila mtu anapenda kufikia. Lakini watu hawa ni lazima blog yako iwe kubwa na kutembelewa mara kwa mara na kila siku angalau na watu 1000 kwa siku.
Lakini pia lazima blog yako iwe imesajiliwa kulingana na sheria za nchi na vibali vingine vya kisheria.
Lakini tukiachana na hilo, unaweza kutafuta matangazo madogo madogo kwa wajasiriamali ambao wametuzunguka kila kona.
Ni vema kuwafahamisha kwanza umuhimu na faida ya kutangaza bidhaa zao na wakaweza kufanya kazi nawe.
Kazi ni kwako kuikuza blog yako na kuanza kuchangamkia fursa hizi za pesa.
Soma na makala hii
2. Kujiunga na Google adsense
Google adsense ni mtandao wa google ambao watu huweka matangazo yao ulimwenguni kote.
Kwa upande wa Google adsense wao huchukua blog ambazo zinachapishwa kwa lugha ya kiingereza tu.
Lakini ipo mitandao mingine ambayo hufanana na adsense na unaweza kutengeneza pesa mara tu baada ya kuunganisha blog yako na mitandao hiyo.
Baadhi yake ni kama vile Propellarads na Adsterra.
Unatakiwa angalau blog yako iwe na watembeleaji wasiopungua 500 kwa siku ili kuweza kuvuna mpunga mrefu.
3. Uza bidhaa zako
Mbali na kutangaza bidhaa za watu, pia unaweza kuwa na bidhaa yako mwenyewe na ukaiuza kupitia blog yako.
4. Uza blog
Kila siku watu wanahitaji kutengenezewa na kudizainiwa blog kwa matumizi mbali mbali.
Unaweza kuanza utaratibu wa kutengeneza blog na kuanza kuziuza kwa watu mbali mbali na kujipatia pesa.
5. Uza maudhui
Hapa unaweza kuandaa Somo muhimu ambalo wahusika itabidi walipie. Hii ni miongoni mwa njia bora zaidi.
Kwa mfano katika nyanja za afya na teknolojia watu wana uhitaji mkubwa sana.
Mbali na hilo pia unaweza kutengeneza vitabu mtandaoni na kuviuza kama soft copy.
Njia zipo nyingi za kuingiza pesa kupitia blog. Lakini hizi ni baadhi ya ambazo nimekuchagulia msomaji wangu.
Kama una swali / maoni / ushauri unaweza kuwasiliana nami kwa namba ambazo zipo sehemu ya contacts au unaweza kuweka comment yako sehemu ya chini ya makala hii.

COMMENTS