Chukua elimu hii kisha mshirikishe na mwingine naye ajifunze

Kijana mmoja aliniuliza "Mbona blog yangu ina muonekano mbaya tofauti na blog nyingine?"
Jibu ambalo nilimjibu kijana huyo ndio makala ambayo nimekuandalia leo nawe msomaji wangu. Huenda nawe ukafaidika kwa makala hii fupi.
TEMPLATE / KIOLEZO
Huu ni mfumo wenye muonekano fulani wa kuipamba blog / website.
Kama unavoiona blog yoyote basi ile ndio inaitwa template. Yapo mamilioni ya tempale ulimwenguni na bado wataalamu wanaendelea kuunda nyingine kadri siku zinavyosogea.
Zipo template ambazo ni maalum kwa ajili ya blog zinazojihusisha na video, maandishi, picha na kadhalika.
Kama ilivyo kwenye upande wa domain, zipo za bure na za kulipia. Basi hata template nazo ziko za bure na za kulipia.
Template za bure ni lazima chini zitakuwa na maelezo madogo ya mtengenezaji. Lakini ukisha nunua inakuwa ni yako mwenyewe hivyo utaiweka kama unavyotaka.
TEMPLATE ZA KULIPIA
Website zinazouza template ni nyingi sana, lakini mimi naupenda zaidi mtandao wa themeforest, colorib na template mag.
Kitu kizuri zaidi ni kwamba template utanunua mara moja tu na hutolipia tena vinginevyo uhitaji template nyingine.
Pia unaweza kuitumia katika blog nyingi bila kulipia tena.
USHAURI
- Chagua template ambayo ni rafiki kwa vifaa vyote vya mtumiaji. Kama vile compyuta na simu ya mkononi
- Angalia template ambayo itaendana na maudhui ya blog yako. mfano;- music video, music audio, movies, maandishi, picha na kadhalika.
- Angalia template ambayo ina maandishi rahisi kwa msomaji wako
- Angalia template ambayo ina share buttons. Hii ni rahisi kwa msomaji wako kuweza kushea makala yako na watu wengine kupitia mitandao ya kijamii. Kama vile facebook, twitter n.k.
- Nunua template kutoka katika mitandao inayoaminika. Hii itakusaidia kupata msaada pale ambapo utahitaji.
- Tumia template ambayo inaruhusu comment.
Bila shaka umepata kitu hapa ee?
Basi niombe maoni yako hapo chini kwa chochote ambacho umeona katika makala hii. Lakini pia unaweza kushea na mwingine naye aweze kupata faida hii.
Asante sana.
Asante sana kwa Mwanga wako
ReplyDeleteAsante Sana kwa kutufuatilia mkuu. Tupo pamoja
Delete