Blog ni jukwaa maalum la mtandaoni ambalo hutumika kuwekwa maarifa na wengine huyapata.

Sasa unaweza kuendelea na kufahamu Idea hizi 10 tu ambazo nimezichuja ili kukunufaisha wewe ambaye unatamani kuanzisha blog lakini hujui azungumzie kuhusu nini.
Ingawa zapo mamia ya idea lakini hizi ni zile ambazo wataalamu wameona kuwa ni bora zaidi kuzifanya kutokana na aina yake pia na umuhimu wake na ufuatiliwaji wake katika jamii tuliyonayo.
NUFAIKA
1. Mtindo wa maisha
Kuna watu wanapenda kuona mitindo mipya ya maisha ya watu wengine ili kujifunza mengi.
Hapa nazungumzia mtindo wa maisha ya kila siku hasa katika matukio ambayo ni vivutio kwa wengine. Kwa mfano unaweza kushea na watu wako safari zako za kuvutia n.k.
Waoneshe watu maeneo ambayo baadhi yao hawayafahamu. Hii wanafanya sana hasa wenzetu ambayo wanaishi nchi za nje.
2. Habari
Habari ni miongoni mwa vyakula muhimu ambavyo mwanadamu ana uhitaji navyo kila siku.
Tunapozungumzia habari tunagusa ulingo mpana sana ambao kamwe hatuwezi kuumaliza. Lakini kwa habari ambazo watu hufuatilia sana ni pamoja na siasa, udaku, michezo na zilizojiri (breaking news)
Ukiweza kuenea katika moja ya nyanja hizo hapo juu basi utakuwa umefaulu. Ni sekta muhimu sana hizo ndugu yangu blogger mwenzangu.
3. Afya
Utakubaliana na mimi kuwa karibu kila mwanadamu ana matatizo. Na huwa anatafuta suluhisho la matatizo yake katika intanet.
Wachukue wenye matatizo na uwalete kwenye uwanja wa blog yako na uwape suluhisho la matatizo zao kwa kuwapa suluhisho la matatizo yao.
Andika makala za afya kadri uwezavyo, andika andika kisha andika tena. Utakuja kunishukuru baadaye.
4. Ushauri
Hapa nazungumzia ushauri wa masuala ya kijamii na maisha ya kila siku. Watu wanatafuta suluhisho la mambo mbali mbali kama vile mahusiano, urafiki hata masuala ya fedha. Hakika watakufuata na kukupenda.
5. Teknolojia
Utaungana nami kuwa siku hizi tunaishi katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Karibu kila mtu anapenda kufahamu mapya kuhusu teknolojia si ndio ee..
Chukua nafasi hii kuwajulisha kile unacho kifahamu kuhusu hili. Wafunze watu mambo yanayohusiana na program za simu, kompyuta na kadhalika. Hakika utakuwa umewakonga nyoyo zao.
6. Mapishi
Hasa akina dada ni watu ambao wanapenda sana kujifunza kuhusu mambo ya mapishi.
Kama unajua kupika itumie fursa hii kuwaelimisha watu. Maana kila siku watu wanapenda kula vyakula vigeni na vyenye ladha tofauti.
7. Muelekeo (Direction)
Aina hii ya idea ya blog haikuenea sana katika nchi zetu za Afrika. Lakini kwa wenzetu ni ishu kubwa tu kwani watu kila siku wanasafiri na kusach maeneo mbali mbali hata kabla ya kufika huko.
Waelekeze watu mahala flani kutoka sehemu flani panapatikana vipi, umbali wake ukoje na jiografia yake.
8. Bidhaa mpya
Kila siku watu wanahitaji kujua kabla ya kununua, kujua kabla ya kuchukua maamuzi ya kuagiza bidhaa mpya.
Lakini pia kuwafahamisha watu kile kipya kilichotoka ili jamii ifahamu yanayoendelea katika masoko.
Lakini kuna mamia ya idea ambazo unaweza kuzitumia kwa ajili ya blog yako na mwisho wa siku kupata mafanikio makubwa. Kwakuwa leo nimeona nikufahamishe hizi 10. Basi zilizobaki kati ya hizo ni pamoja na;-
9. Urembo na
10. Fursa za ajira (mbali mbali)
Je? Una maoni yoyote? Basi tuandikie hapo chini sehemu ya comment.
****************
*******************

COMMENTS