
Wislamumu Mkoani Mbeya wameungana na Waislam wote Tanzania na Duniani kote katika kusherehekea sikukuu ya Iddi Alfitri.
Ibada ya Iddi Alfitri hufanyika mara tu baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Waislamu jijini Mbeya wamekamilisha kwa amani na utulivu katika viwanja vya SOKOINE jijini humo.
Viongozi wa dini na serikali kwa ujumla walihudhuria ibada hiyo huku mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa ndg Albert Chalamila.
Akizungumza na waumini baada ya Swala kumalizika Chalamila aliwapongeza Waislam kwa kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wakiwa na afya njema.
Lakini pia aliwahakikishia usalama wao na mali zao katika siku hii.
Chalamila aliendelea kuwaambia waumini na wananchi wote kuwa wawe wavulivu kwa muda mchache kutokana na changamoto ya usafiri iliyojitokeza baada ya madereva wa daladala kugoma.
Aliwaahidi kulishughulikia suala Hilo ndani ya siku chache zijazo.
Mbali na mkuu wa Mkoa, pia sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ndugu Msafiri Njalambaha alizungumza machache na kuwahimiza waumini kuendelea na uchamungu wao ambao wameondoka nao Mwezi wa Ramadhani.
Ibada hiyo ilikamilika mnamo majira ya saa 3.30 asubuhi kwa kufanya harambee ya michango ya maendeleo mbali mbali ya Dini.
Chini ni baadhi ya picha za tukio zima ibada hiyo tukufu.
![]() |
| Waumini wakiendelea na takbira wakisubiri Swala ya Iddi |
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ALBERT CHALAMILA akiongea na waumini |
![]() |
| Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba za viongozi mbali mbali |




COMMENTS