Huwezi kutaja mikoa maarufu Tanzania na kuuacha Mkoa wa Mbeya. Hii ni historia yake kwa ufupi
JINA LA MKOA LA MBEYA
Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni (Waingereza) mnamo mwaka 1927.
Enzi za ukoloni wa Waingereza, Mkoa wa Mbeya ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’.
Mkoa ulikuwa ukiunganisha baadhi ya maeneo ya mikoa mitatu ya sasa ambayo ni Iringa na Rukwa.
Jina la Mbeya limetokana na neno la kisafwa."IBHEYA" ambalo maana yake ni chumvi, hii ni kutokana na wafanyabiashara kufika na kubadilishana mazao yao kwa chumvi (butter trade).

Kutokana na hali nzuri ya hewa ilisababisha mji wa Mbeya kupewa jina la utani kama "The Scotland of Africa" baada ya kutambua kama uoto, hali yake ya hewa na muonekano wa milima (hills) inayouzunguka mji wa Mbeya kufanana na Scotland.
Uoto unaopatikana katika mlima Loleza. Mkoa huu ni moja kati ya mikoa mikongwe sana hapa Tanzania.
Katika kipindi hicho, makabila makuu katika Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni Wasafwa, Wanyakyusa, Wandali, Wasangu, Wamalila, Wanyiha, wakimbu na Wanyamwanga. Ambapo jamii hizo ni maarufu kwa kujishughulisha na kilimo na ufugaji mdogomdogo.
COMMENTS