Huu ni MOJA katika magonjwa ambayo huwatesa Sana wazee na watoto.

Neno pumu maana yake ni ugumu wa upumuaji katika njia ya kawaida, mgonjwa hupumua kwa mdomo au pua kupitia katika miriija ya hewa na kusafiri katika mapafu.
Mtu mwenye afya hupumua kwa sekunde 16 hadi 18. Wakati kwa watoto ni sekunde 20 hadi 25.
Lakini kwa mgonjwa wa pumu ni tofauti kwani hupumua kwa shida na sauti ya kukoroma.
Ziko aina mbili za ugonjwa wa pumu
- Pumu ya Koromeo
- Pumu ya moyo
VISABABISHI VYA KUPATA PUMU
1. Mzio (Allergy)
Mzio ni aina ya makatazo katika mwili. Mfano unaweza kuwa aina ya vyakula, manukato n.k.
Hii ni moja kati ya vitu ambavyo huweza kusababisha ugonjwa huu pale ambapo mtu atakiuka mipaka ya mzio alionao.
2. Kurithi
Hii ni sababu kubwa ya kupata pumu. Kama historia ya ukoo wenu inaonesha kuwa babu/baba zako walisumbuliwa na pumu nawe ni lazima utaipata.
3. Sababu za kisaikolojia
Hizi ni sababu ambazo huletwa na mihemko hasi kama vile hasira, wivu, ugomvi na vingine vinavyofanana na hivyo.
Mtu mwenye matatizo hayo ni rahisi sana kupata pumu kwa sababu ya kutokuwa na muda wa kuvuta pumzi zaidi ya ugomvi na chuki.
4. Mabadiliko ya hali ya hewa
Pumu inaweza kutokea baada ya hali ya hewa kubadilika kama baridi kali au mvua.
Baridi inapopiga katika mapafu husababisha mishipa ya damu isiingize oksijen ya kutosha. Hatimaye hewa hupungua katika koromeo na kupata shida hii ya kupumua.
5. Mtindo mbaya wa maisha
Baadhi ya vyakula vinaweza kusababisha ugonjwa wa pumu. Kama vile;
- Kula vyakula vilivyokobolewa. Kama sembe, ngano nyeupe n.k
- Kukla vyakula vyenye mafuta mengi
- Kukaa sehemu zenye hewa chafu na harufu mbaya kama viwandani n.k
DALILI ZA UGONJWA PUMU
Hizi ni baadhi ya dalili zake
- Kifua kubana
- Mapigo ya moyo kwenda mbio
- Kuhisi baridi
FANYA MAMBO HAYA KWA MGONJWA WA PUMU
- Pindi uamkapo asubuhi usitoke nje mabega wazi. Jifunike mwili wako, hasa kama unaishi katika maeneo ya baridi kali.
- Usioge maji ya baridi katika kipindi cha baridi
- Usitembee peku peku, wala kuvaa viatu vya wazi. Vaa viatu vya kufunika miguu kama buti, raba ikiwezekana na soksi.
- Kaa mbali na moshi, vumbi. Pia kaa mbali na mtu anayevuta sigara
- Usilale mara tu baada ya kumaliza kula. Subiri yapite walau masaa mawili ndipo ulale.
TIBA YA PUMU
- Kunywa maji ya uvuguvugu yaliyowekwa limao
- Weka mfuko wa maji ya moto kifuani na tumboni
- Kunywa chai ya mchaichai iliyowekwa tangawizi
- Fanya massage sehemu ya kifua, tumboni na mgongoni
COMMENTS