Kama kuna tours ambazo sitozisahau kwa sababu ya uzuri wake basi ni hii.
Tunafanya kazi sana, tunasoma sana, tunajishughulisha na mambo mbali mbali. Lakini kuna muda tunatakiwa kuenjoi na kufurahi na familia zetu kwa kubadilisha mazingira na kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii.
Jumapili ya leo tunaburudika na Wanafunzi wa madrasat Tawfiq iliyopo SOWETO - MBEYA ambao waliandaa tour ya kuelekea eneo la VIEW POINT lililopo hapa mkoani mbeya.
Sheikh Hassan Mbarazi ndiye Mudiri na kiongozi wa madrasa hiyo, akiambatana na uongozi wake huo sambamba na sisi BUNDUKI MEDIA tulianza safari majira ya saa 4 asubuhi eneo la Masjid Tawfiq Soweto.
Na safari ilikuwa kama hivi;-
Hawa ni wanafunzi na Viongozi wa Madrasati Tawfiq wakipata picha dakika chache kabla ya safari.
View point ni eneo la barabara lililoko juu kuliko meneo yote Tanzania. Eneo hili hupatikana takriban kilomita 25 kutoka katikati ya jiji la Mbeya kuelekea Wilayani Chunya.
Ukiwa hapo utaona mandhari yote ya jiji la Mbeya ikiwa kwa mbali mno na kwa chini sana. Eneo hili hufurahisha sana macho ya mtazamaji. Mbali na jiji la Mbeya lakini pia unaliona kwa ukaribu bonde la Usangu ambalo lipo kwa mbali na kwa chini zaidi.
Ikumbukwe tu haya ni maeneo ambayo yamepitiwa na bonde la ufa hivyo hiyo ni miongoni mwa sababu za kuifanya sehemu hii kuvutia zaidi.
Watu wengi huenda kutalii eneo lile kwa ajili ya kupunga upepo mwanana, lakini pia baadhi yao huandaa matamasha mbali mbali na kwenda kuyafanyia kule ikiwa ni sehemu ya kujifunza na kufurahia maumbile ya Mwenyezimungu.
Kwa upande wa Madrasat Tawfiq wao waliandaa mambo kadhaa ikiwemo michezo kwa watoto kama vile kushindana kukimbia, kukimbia na magunia na mpira wa miguu.
Michezo ambayo ilitanguliwa na mafunzo ya vitendo ya swala ya safari na swala wakati wa vita.
Endelea kufurahia picha hizi nzuri maeneo hayo;-
 |
Muonekano wa bonde la usangu Ukiwa juu |
 |
Mafunzo kwa vitendo - Swala ya safari |
 |
meckpro - Camera man (Bunduki Media) |
 |
Katibu wa wanafunzi (Salum) Akisoma risala Maalum |
Baada ya pirika zote kuisha, watu waliandaliwa chakula kabla ya kuanza safari ya kurudi kuelekea Mjini Mbeya.
 |
Pichani ni wanafunzi wakipata chakula cha mchana |
Huu ndio ulikuwa mwisho wa Tour yetu. Ungana nasi katika mitandao yetu ya YOUTUBE, na BLOG ya mrbunduki.com kwa ajili ya kupata matukio haya kila yanapopanda hewani.
COMMENTS