Vihatarishi vya maambukizi ya fangasi ukeni ni vingi sana ambavyo ni pamoja na mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambao husababisha mabadiliko kati
Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua tatizo kubwa sana Duniani. Asilimia 75 ya wanawake wote duniani wanasumbuliwa na tatizo hili.
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na fangasi wanaoitwa CANDIDA ALBICANS, maambukizi haya pia hujulikana kama YEAST INFECTIONS / THRUSH
CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia Chakula (PHARYNX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke.
Bacteria Hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika yanayojadiliwa, Mfano mabadiliko katika hali ya PH, yanayosababishwa na matumizi ya MADAWA ya antibiotics, pia kupungua kwa kinga kutokana na magonjwa tofauti.
Vihatarishi vya fangasi ukeni
Vihatarishi vya maambukizi ya fangasi ukeni ni vingi sana ambavyo ni pamoja na mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambao husababisha mabadiliko katika sehemu za siri pia vihatarishi vingine ni hivi;-
- msongo wa mawazo
- utapiamlo (malnutrition)
- matibabu ya homoni(hormonal replacement therapy)
- ujauzito
- kujamiiana kinyume na maumbile/kwa njia ya haja kubwa (anal sex
- matumizi ya glycerin wakati wa kujamiiana
- kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sehemu za siri
- matumizi ya dawa za uzazi wa mpango
Dalili za ugonjwa wa fangasi ukeni
- Kuwashwa sehemu za siri
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa (superficial dysapareunia)
- Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
- Kupata vidonda au michubuko ukeni (soreness)
- Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje wa uke (Labia minora)
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa
- Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mzito, mwepesi au majimaji.
Matibabu na jinsi ya kujikinga
Ugonjwa huu wa fangasi matibabu yake hupatikana kwa urahisi.
Tanzania na tiba hupatikana na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi na majibu yaliyotoka, pamoja na hayo ugonjwa huu unazuilika hivyo njia nzuri ni kujikinga kwa kufanya yafuatayo;-
- Vaa nguo za ndani (chupi) ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri epuka synthetic underwear, pia epuka kuvaa nguo za ndani za mtumba.
- Epuka kufanya mapenzi yasiyo salama na mpenzi wako mwenye maambukizi haya.
- Kula mlo wenye virutubsho.
- Epuka kuoga maji ya moto (hot baths) kipindi cha joto tumia maji ya vuguvugu
- Osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji safi na sabuni za asili na tumia kitambaa kisafi kujikausha maji.
- Epuka matumizi ya vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys)au vifaa vya kupanga uzazi (diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi.
- Tumia pads nzuri
- Kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture mara kwa mara kwani husaidia kuepusha maambukizi haya
- Epuka kutumia sabuni zenye manukato kama vile bath powder, feminine hygiene, bubble baths, vaginal deodorant.
COMMENTS