Ni ndoto ya kila mtu kukua na kuwa maarufu katika kazi yake ya blooging. Basi kwa kuwekeza katika mambo haya 6 utafanikiwa katika hilo.

Kila blogger anatamani siku moja tu aamke akiwa maarufu na blog yake iwe na watembeleaji wengi kuliko blog zote. Anatamani kuwa kioo cha jamii nchihi barani na Duniani kote.
Kama nawewe ni mmojawapo basi hili linawezekana lakini ni lazima uwekeze katika mambo haya 6 muhimiu.
Mwandishi ni Saidi Bunduki
1. Elimu
Wekeza zaidi katika kujifunza juu ya kile ambacho unafanya. Bila shaka utakubaliana na mimi kuwa ulimwengu unakwenda kasi na mambo kila siku yanabadilika na kuendelea.
Jifunze kutoka kwa watu, bloggers maarufu, mitandao mbali mbali ya nje na ndani ya nchi jinsi ya utendaji kazi katika kile unachokisimamia.
Muonekano wa blog, domain bora, logo na spidi ni vitu vya kuzingatia sana.
Soma makala hii ambayo itakuwa msaada kwako
Fahamu kuhusu template (muonekano wa blog)
Laa sivyo utabaki ulipo na hutoweza kupiga hatua.
2. Nguvu kazi
Kuna muda utafika ili upige hatua ni lazima uwe na msaidizi / wasaidizi. Waswahili walishasema 'Kidole kimoja hakivunji chawa'
Tafuta wataalamu wa kada mbali mbali kulingana na aina ya blog yako. Wataalamu wakusaidie katika kuandaa kitu ambacho kitakuwa ni bora, kukupa ushauri na kukupa moyo pia.
Wekeza katika kuitangaza blog yako katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Hapa pia huhitaji msaada mkubwa kutoka katika makundi mbali mbali ya watu jambo ambalo wewe mwenyewe ni gumu kulifanya.
Kitu kingine muhimu zaidi wekeza katika vifaa vya kazi. Ni lazima uwe na vitendea kazi vyenye ubora wa hali ya juu mfano computer, camera, program zinazoendana na kazi yako na kadhalika.
3. Muda
Ukitaka mafanikio makubwa ya haraka katika jambo lolote ni lazima kujali na kuzingatia rasilimali muda.
Hapa itakulazimu muda wako mwingi kuutumia katika jambo hili. Utatakiwa uwe tayari kuvunja baadhi ya ratiba kwa sababu ya kublog.
Usiku ni muda mzuri zaidi wa kuandika kwa kuwa akili inakuwa imetulia na unaweza kufanya kitu bora zaidi.

4. Saidia watu
Hata kama wewe ni mdogo basi kuna mdogo zaidi yako. Watakuja bloggers wadogo zaidi yako kwa lengo la kupata msaada wako. Wape msaada bila kujali. Kwa sababu ya baraka zao na kukubali kwao wewe ni sababu ya wewe kubarikiwa na kufika mbali zaidi.
Saidia watu katika makala zako unazoandika. Makala ziwe na msaada kwa msomaji kulingana na niche (idea) ya blog yako.
Kama wewe ulivopata msaada kupitia makala hii.
Soma pia
5. Uvumilivu
Kuwa mstahamilivu katika kila jambo. Watu watakucheka, kukudharau na kuona unapoteza gharama kubwa bila faida. Simamia katika unachokiamini na usiwasikilize kamwe.
Uvumilivu pia katika yote tuliyo yaorodhesha hapo juu na mengine ambayo hatujayataja.
6. Muombe Mungu
Point hii nimeiweka ya mwisho ingawa ilitakiwa kuwa ya kwanza.
Mtegemee, muomge na umshukuru Mungu kwa mujibu wa imani yako. Kwani tunaamini hakuna mafanikio bila ya majaaliwa ya Mwenyezimungu.
Baada ya jitihada za kibinadamu, ni lazima kumuelekea yeye kwa kuhitaji na kuomba msaada wake.
Hadi wakati mwingine nakutakia siku yenye baraka na mafanikio maishani mwako.
COMMENTS