Astaghfirullaahi waatuubu ilaika
1 *Katika faida kubwa ya KUSTAGHFIRU ni kuwa unatekeleza ibada ya kumuabudu Mola wako mlezi ambae amekuumba na amekupangia maisha na uhai wako wote..*
2. *Vilevile ni kufuata mwendo wa Mtume wetu SAW ambae alikuwa ANASTAGHFIRU zaidi ya mara sabini kwa siku..*
3. *Ni ibada nyepesi ambayo haina masharti maalumu ya udhu, wala mahala, wala usafi.. unaweza kuifanya wakati wowote mahala popote katika hali yoyote..*
4. *Unapomtaja Mungu kwa wingi katika KUSTAGHFIRU kwako, inapelekea Allah kuwa karibu zaidi na wewe*
5. *KUSTAGHFIRU kunaleta utulivu katika moyo, na unajisikia kuridhika na hali uliyonayo.. pamoja na bishara njema zinazoletwa na matarajio ya kusamehewa madhambi yako..*
6. *Watu wanapokaa na KUSTAGHFIRU kwa nia nzuri na ikhlasi ya kweli, kisha wakamuomba Allah chochote hukubaliwa maombi yao*
7. *Kama unataka kupata mtoto wa kheri, au kupata riziki nzuri, kupata mvua zenye baraka... yote hayo huletwa kirahisi endapo imedumishwa ISTIGHFAR..*
8. *ISTIGHFAR inaondosha mabalaa na majanga mengi sana ambayo yalikuwa yakufike.., na inakuletea afya njema na siha kamili ya mwili wako..*
9. *Ikiwa unasumbuliwa na maradhi ya Mabilisi au kuna maradhi yoyote yaliokuwa hayasikii dawa.., endelea kudumu na ISTIGHFAR utaona matokeo yake..*
10. *Kama unataka mafanikio ya jambo lolote la kheri.., (ndoa, biashara, ajira, masomo..nk) unatakiwa KUSTAGHFIRU sana halafu omba ukitakacho*
Kustaghfiru ni kusema:
*(ASTAGHFIRULLAHAL ADHIIM)*
*(RABBIGHFIR LII WATUB ALEY INNAKA ANTA TTAWWABU RRAHIIM)*
TUJITAHIDI KULETA ISTIGHFAR MWENYEEZI MUNGU ATUSAMEHE NA ATUPE KILE TUNACHO KIHITAJI SEMA AMIN
COMMENTS